← Back to list

USIPOUTUMIA UJANA, UZEE UTAKUTUMIKISHA

Nilimkuta kajiinamia, akiwa na mawazo mengi. Kichwa chake kimebebwa na mikono iliyokuwa juu ya mapaja yake. Nilipomtazama, macho yake…

Nickson Kisinga · 2022-03-16 20:01 · 0 claps · 2.1 min read
#real-estate #tanzania #nyumba #uchumi #real-estate-agent
Open on Medium ↗
Wiki topics: AGT · AI Agents PFI · Personal Finance

USIPOUTUMIA UJANA, UZEE UTAKUTUMIKISHA

Nilimkuta kajiinamia, akiwa na mawazo mengi. Kichwa chake kimebebwa na mikono iliyokuwa juu ya mapaja yake. Nilipomtazama, macho yake yalilengwa na machozi, sura yake ilionekana kana kwamba amepata msiba mzito na sasa amepoteza tumaini.

Alikuwa ni mzee Ngoswe, alinijulisha jina lake baada ya kumsalimia na kuhitaji kujua ni Maswahibu gani yamemkuta mpaka kuwa katika hali ile,

Ilikuwa ni chini ya mti, amekalia kipande cha tofali la Cement au la block kama wengi tunavyoita

Mbona upo kwenye hali hii mzee wangu? Niliuliza

Akasema mwanangu kaa chini hapo kwenye tofali hilo nikusimulie usije rudia makosa niliyo yafanya nilipokuwa na nafasi na uwezo,

Nilisogeza tofali lile nikachukua leso yangu na kulifunika ili suruali yangu isichafuke maana nilikuwa bado na mizunguko ya siku, nikaketi tofalini na kuanza kumsikiliza! Fuatilia sasa simulizi yake...

"Nilikua ni mtu mwenye uwezo mkubwa serikalini, nikiwa nimeajiliwa katika shirika moja la Uma hapa nchini, nilikuwa mkurugenzi wa kanda na mikoa kadhaa ilikuwa ikiripoti kwangu.

Mshahara ulikuwa ni mkubwa kwakweli, posho na fedha ya mawasiliano ilikuwa kubwa mara tano zaidi ya mshahara wa mlinzi wa shirika.

Kwa kifupi fedha nilikuwa nayo mwanangu,

Pamoja na kuwa na fedha nyingi lakini pia nilikuwa mtu wa starehe baada ya kazi ilikuwa ni kwenda kula maisha na rafiki zangu, mimi ndiyo nililipa bill zote, mara kadhaa niliamuru mziki uzimwe bar na nikachagua wimbo ninaoupenda na kulipia wimbo huo, hakuna aliyethubutu kunibishia kwani jeuri ya fedha ilitawala. Sikupenda binti mrembo yoyote akatize mbele yangu bila ya kumuhitaji kwa gharama yoyote, japo nilikuwa na mke wangu lakini niliamini fedha ninazomuachia zinamtosha hivyo sikusumbuka naye. Kila wikiendi ilikiwa ni kama sherehe kwangu na rafiki zangu, fedha iliteketea lakini sikujali wala kushtuka.

Hakuna lolote la maendeleo nililolifanya zaidi ya starehe.

Ilibaki miaka miwili ya kukaribia kustaafu ndipo Nilipo anza kutafakari nitaishije nikiwa sina hii ajira? Ila nilijipa moyo kwani kiinua mgongo changu niliamini kingekuwa kikubwa na ningeweza kukitumia kuweka mambo sawa na kuishi maisha mazuri ya uzee, NILIJIDANGANYA...

Ukweli nilistaafu na nilipata kiinua mgongo changu Milioni mia moja na sehemu, Nilinunua gari nzuri kwanza ya kutembelea, halafu iliyobaki nikaanza ujenzi, kuja kutahamaki ujenzi haujaisha na bado fedha inahitajika sababu pia sikuwa na uzoefu wa ujenzi hivyo ramani na uhalisia ulikuwa ni vitu tofauti nyumba ilikuwa kubwa na gharama zilikuwa juu sana!

Gari niliyonunua ilibidi niiuze ili nimalizie nyumba, baada ya nyumba kuisha sina fedha na maisha yanabidi yaendelee, kulikuwa na kaakiba kadogo nikakatumia kuanza biashara, ilinifanye vizuri nikakopa bank kuongeza mtaji, kwa sababu sina uzoefu wa biashara, nayo ilinishinda na bank waliuza nyumba yangu sababu sikuweza kulipa mkopo ule. Hapa sina mbele wala nyuma na sielewi nafanya nini. Ujana nilichezea na fedha nilitapanya sikujua kama ntafika kwenye nyakati kama hizi! "

Nilimpa moyo mzee huyu na kumwambia kwamba anaweza kuanza upya japo amechelewa sana. Baadae alipata kazi ya ulinzi kwenye kampuni fulani na mpaka sasa anafanya huko, maisha anayoishi ni ya majuto kwa muda na fedha na rasilimali alizo poteza kwa starehe wakati akiwa na nguvu!

SIKILIZA Unaweza kuepukana na yaliyomkuta mzee huyu kwa kufanya maandalizi yako mapema kimaisha.…


메타데이터
post_id
26f5cc0b888d
slug
usipoutumia-ujana-uzee-utakutumikisha-26f5cc0b888d
url
https://medium.com/@kisinganickson/usipoutumia-ujana-uzee-utakutumikisha-26f5cc0b888d
canonical_url
https://medium.com/@kisinganickson/usipoutumia-ujana-uzee-utakutumikisha-26f5cc0b888d
author_url
https://medium.com/@kisinganickson
status
ok
fetched_at
2026-07-27 09:30:34