← Back to list

KASUKU MNENAJI

Shairi la ki-leo

Msafiri R. Ulimali · 2024-01-15 10:19 · 1 claps · 0.7 min read
#swahili #poem #shairi
Open on Medium ↗
Wiki topics: LIT · Literature & Writing ✍️ · Writing & Creative 💄 · Beauty

KASUKU MNENAJI

Shairi la ki-leo

Mimi ni kasuku mnenaji niliyefungiwa kwenye banda la dhahabu,

maneno yangu matamu nikiwa ndani, mbawa zangu zameremeta

Nikiamka asubuhi nawadhiaki walio nje, na kuwaona hawafai

Kasuku mwenye mikogo, lakini nimefungwa yangu miliki mdomo

Angali mbawa zangu zikiwa ndogo, nilketi nao nje

Tulinena makuu, mabadiliko ya nchi

Fikra zangu silaha, zapotelea kwenye banda la dhahabu

nimekuwa kibogoyo, nikiogopa patilizwa na wenye meno

Sasa nipo ndani wananipitishia vitamu, ila kero yangu matusi

Banda langu la thamani, hata kinyaa sikioni

Wao waniita mfungwa, ni wivu wananionea

Shaba hawana, dhahabu yangu dhihaka

Wanitazamapo hudhuni uwajia, mwenyewe sina habari najionea fahari

Uzio wangu wasafishwa kila siku, macho yajaa ukungu

Sioni ya kwao, wanayaona ya kwangu

Banda langu la thamani, lasimamisha fikra zangu

https://twitter.com/MyHadithi/status/1585936939273723905/video/1


메타데이터
post_id
72a249dd78fc
slug
kasuku-mnenaji-72a249dd78fc
url
https://medium.com/@msafir/kasuku-mnenaji-72a249dd78fc
canonical_url
https://medium.com/@msafir/kasuku-mnenaji-72a249dd78fc
author_url
https://medium.com/@msafir
status
ok
fetched_at
2026-07-24 14:22:46